Tuesday, May 19, 2015

MAJESHI YA MUUNGANO YASHAMBULIA YEMEN

Majeshi ya muungano yashambulia Yemen

Ndege za kijeshi za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zamefanya mashambulizi dhidi ya Houthi nchini Yemen
Habari kutoka mji mkuu wa Yemeni - Sanaa, zasema kuwa kumetekelezwa mashambulio makali ya angani.
Inasemekana kuwa ndege za majeshi ya muungano yakiongozwa na yale ya serikali ya Saudi Arabia, zinarusha makombora makali, tangu kumalizika kwa siku ya mwisho ya usitishwaji wa mapambano hapo siku ya Jumapili.
Ndege hizo za kivita zinalenga maeneo muhimu yalio na waasi wa Houthi na washirika wao.
Mashambulizi ya angani pia yameripotiwa katika mataifa kadhaa ya Yemen, ikiwemo mji wa Aden, kusini mwa taifa hilo.

No comments:

Post a Comment