Tuesday, May 19, 2015

MAREKANI KUREJESHA MAGARI MILIONI 30 VIWANDANI

Marekani yabaini kasoro katika magari

Mifuko ya Hewa ya Kampuni ya Takata ikiandaliwa kiwandani tayari kwa matumizi
Karibu magari milioni thelathini na nne yanarejeshwa viwandani nchini Marekani ambako mifuko ya hewa ya usalama katika magari imelalamikiwa kusababisha vifo vya watu wapatao watano.
Tukio hili la urejeshwaji wa magari viwandani kutokana na kasoro za kiufundi ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani. Kampuni ya kutengeneza vifaa vya magari ya Japan, Takata, imekiri mifuko ya hewa kulinda usalama wa watumiaji wa magari kuwa na kasoro. Baadhi ya mifuko hiyo ya hewa imepasuka kwa nguvu kupita kiasi na kusababisha kurusha vipande vya chuma kwa madereva na abiria wanaokaa viti vya mbele. Waziri wa Usafirishaji wa Marekani, Anthony Foxx, ametangaza kurejeshwa kwa magari yenye hitilafu ya mfumo huo kote nchini humo.
Mfuko wa hewa ukifyatuka wakati wa ajali kumlinda mtu aliye ndani ya gari.
 Foxx amesema urejeshwaji wa magari hayo ni kazi kubwa.
Tangazo hilo limetolewa na Utawala wa Usalama wa Taifa nchini Marekani katika Barabara Kuu baada ya mazungumzo marefu na kampuni ya Takata. Magari yanayorejeshwa yanahusu kampuni kumi na moja za kutengeneza magari zikiwemo za Honda, Toyota na Nissan.
Urejeshwaji viwandani kwa magari mapya hufanyika baada ya kugundulika hitilafu lolote la kiufundi linaloweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa magari hayo.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakato wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment