Tuesday, May 19, 2015

WAHAMIAJI KUJADILIWA MALAYSIA

Wahamiaji kujadiliwa,Malaysia

Mawaziri wa mambo ya nje wa Thailand,Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa dharura mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika ukanda wao.
Nchi hizo tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya wahamiaji waliokwama Baharini ambao wanahitaji chakula na maji.
Wahamiaji wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar, lakini Serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo.
Wavuvi nchini Indonesia wamewaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano
Bado kuna hofu kuhusu usalama wa waliokwama baharini.Maelfu ya Raia kutoka Bangladesh na Waislamu jamii ya Rohingya wamekuwa katika bahari ya Andaman kwa majuma kadhaa sasa.
Thailand,Malaysia na Indonesia zimekataa kuwaruhusu kuingia katika pwani za nchi zao
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowowte kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment