Saturday, May 16, 2015

MAREKANI YAIPA SOMO CHINA

Kerry aitaka China kupunguza misukosuko


Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry amezumgumzia misukosuko inayozidi kuongezeka kusini mwa bahari ya China alipokutana na viongozi wa vyeo vya juu wa chama cha Kikomisti mjini Beijing.
Ameitaka China kuchukua hatua ili kupunguza misukosuko eneo hilo. Marekani inasema kuwa China imejenga miradi ya ardhi ya karibu ekari 800 kwenye visiwa vya Spratly mwaka mmoja uliopita.
Nazo meli za jeshi la marekani zimekuwa zikipiga doria kwenye visiwa vya spatry ambavyo vinadaiwa na china na nchi zingne tano.
China inaamini kuwa Marekani inazichochea nchi za Asia kukabiliana nayo katika kudai maeneo ya bahari.
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment