Friday, May 8, 2015

PELE AFANYIWA UPASUAJI WA KIBOFU CHA MKOJO

Hospitali imeamua hivi kuhusu afya ya mkongwe wa soka duniani Pele..

pele
Baada ya aliyekuwa nyota wa timu ya Taifa ya Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele kuugua kwa muda wa miezi sita, hatimaye uongozi wa hospitali ya Sao Paulo, Brazil imefikia maamuzi ili kuokoa maisha yake.
Wataalam wameamua kumfanyia Pele upasuaji wa kibofu cha mkojo katika hospitali hiyo ili kuondoa mawe yaliyokuwa yakimsumbua katika figo yake
Pele mwenye umri wa miaka 74 alilazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita.
Pele ambaye jina lake ni Edson Arantes do Nascimento alifunga zaidi ya mabao 1200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia Brazil kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukusogezea muda na wakati wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment