Thursday, May 14, 2015

WAFANYUABIASHARA WENYE MADUKA TANGA WACHARUKA



Tangakumekuchablog

Tanga, WAFANYABIASHARA wenye maduka jijini Tanga, wametishia kufunga maduka yao ikiwa Kikosi Cha Zima Moto na Uokozi kitaendelea kuwabughuzi wafanyabiasha hao kwa kuwataka kuweka kifaa maalumu cha kuzimia moto(Fire Extingsher).

Wakizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara ulioitishwa kufuatia kikosi hicho kupita madukani kuwataka kuweka  kifaa hicho na kufunga  maduka, wamesema endapo wataendelea   watafunga maduka yao na kufanya mgomo.

Wamedai  sheria hiyo ni kandamizi na hivyo kukitaka kikosi hicho kuacha mara moja kuwabughuzi wafanyabiasha na badala yake kuangalia changamoto zinazowakabili.

Wamesema kikosi hicho kiko na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa magari na maji ya kuzimia moto na kuchelewa kufika kwa wakati maeneo ya matukio .

Tangakumekuchablog ilifanya jitihada za kuzungumza na kamanda wa kikosi cha Zima Moto Tanga, kuzungumzia malalamiko hayo lakini ilishindikana na kuelezwa uongozi uko katika kikao.

                                                       Mwisho

No comments:

Post a Comment