Friday, May 8, 2015

WATU 12 WAOKOLEWA DAR

WATU 12 WAOKOLEWA BAADA YA NYUMBA ZAO KUZINGIRWA NA MAJI ENEO LA KINONDONI MKWAJUNI JIJINI DAR



Watu takribani 12 wamearifiwa kuokolewa kutoka ndani ya nyumba zao baada ya kuzingirwa na maji eneo la Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa. Zeozi hili la uokozi limefanywa na kikosi cha zima moto kutoka Ilala pamoja na vijana wa skauti.


Licha ya zoezi hilo kupata mafanikio kwa kuokoa watu wote ambao afya 
zao zilikuwa salama vurugu pia zilijitokeza baada ya kundi moja la vijana kupinga zoezi hilo bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi na kubainika kuwa walikuwa na lengo la kupora.

No comments:

Post a Comment