Wednesday, May 13, 2015

WAZIRI WA ULINZI KOREA KASKAZINI AUWAWA KWA KOMBORA

Kifo cha Waziri wa Ulinzi Korea Kaskazini kisa kasinzia mbele ya Rais.

koreSerikali ya Korea Kaskazini imeingia kwenye Headlines…Ni baada ya Waziri wake wa Ulinzi Hyon Yong-chol kuuawa wakati kiongozi wake nchi hiyo Kim Jong-un alipokuwa akiwahutubia kwenye kambi ya kijeshi.
woteTaarifa iliyotolewa na Bunge la nchi hiyo inasema Waziri huyo alikumbwa na umauti baada ya kupigwa na kombora la kivita la kuangusha ndege mbele ya maafisa wakuu wa Serikali wakati aliposinzia wakati mkutano huo ukiendelea.
Inasemekana alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na Rais wa nchi hiyo jambo ambalo lilimuudhi Rais huyo.
Hyon Yong-chol aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Korea Kaskazini  mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment