Wakazi wa Amboni Tanga wakipita
daraja la mbao la majimoto ambalo chini kunadaiwa kuwa na mamba wakali, Daraja
hilo limejengwa toka enzi ya wakoloni wa Kijerumani na kutumika hadi sasa.
Inasemekana mamba hao wamekuwa wakionekana nyakati za asubuhi na jioni na kuzusha kitisho kwa watumiaji wa daraja hilo ambalo ni la mbao.
Hata baadhi ya watu wameiambia tangakumekuchablog kuwa toka kugundulika mamba hao hakuna mtu yoyote ambaye aliwa mbali ya kujeruhiwa mwanzoni mwa miaka ya 90.
Inadaiwa kuwa mtu huyo aliejeruhiwa alikuwa akifua nguo na kushtukia kunyofolewa mkono wake wa kushoto na mamba kutokomea kwenye kina kikubwa cha maji.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment