Marekani yakana kuhusika na mapinduzi Uturuki
i
Marekani imeitaka
Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya
Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.
Bwana Gulen anayakana hayo.
Mapema nchini Uturuki maelfu ya watu walijitokeza wakiimba na kupeperusha bendera ya taifa katika barabara za mji wa Istanbul na Ankara kumuunga mkono rais Erdogan.
Serikali imetawaka wafuasi wake kusalia katika bustani kuu usiku kucha. Mashirika kadha ya ndege yalirejea safari zao kwenda Istanbul Jumamosi jioni.
BBC
No comments:
Post a Comment