Ndege ya kisasa ya Ethiopia yatua Kenya


Ethiopia imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kununua ndege ya kisasa aina ya Airbus A350 XWB.Ndege hiyo, iliyo na uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 300, ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano jioni ikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ndege hiyo ni ya kwanza kuwasilishwa kwa kampuni hiyo, huku nyingine 13 ilizoagiza kutoka kwa kampuni ya Airbus zikisubiriwa hivi karibuni.
Safari ya kwanza ya ndege hiyo ilifanyika tarehe 2 Julai iliposafiri kutoka Ufaransa hadi mjini Lagos, Nigeria.
Kampuni ya Ethiopian Airlines inaorodheshwa ya kwanza barani Afrika kwa faida na pia idadi ya maeneo inayosafirisha abiria.
No comments:
Post a Comment