Taiwan yarusha kombora la kulipua meli kimakosa
Jeshi la wanamaji la Taiwan limezindua kimakosa kombora la kulipua meli kutoka kambi yake ya Kaohsiung, maafisa wanasema.
Boti moja iliokuwa ikipiga doria ilikuwa inafanyiwa zoezi la ukaguzi wakati kombora hilo Hsiung Feng 3 liliporushwa .Kombora hilo lilianguka katika maji ya kisiwa cha Penghu karibu na China lakini halikusababisha madhara yoyote.
Kisa hicho kinajiri wakati ambapo China inasheherekea maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa chama cha Kikomyunisti.
Alisema kuwa kisa hicho kinachunguzwa na kitaangaziwa vilivyo.
Haijulikani iwapo Bejing ilijulishwa.
Kombora hilo linaweza kurushwa umbali wa kilomita 300.China inaichukulia Taiwan kama mkoa wake uliojitenga.
BBC
No comments:
Post a Comment