
Nimekuwekea leo kutoka kwenye show ya XXL na story ya kwanza kusikika inamhusu mwanamziki mkongwe
Daz Baba
ambaye amezungumzia ishu ya familia yake na kusema kuwa kwa sasa
anaishi peke yake na anahangaika kwa ajili ya kuwatengenezea maisha
watoto wake wawili ambao wanasoma, amekuwa akiwatembelea mara kwa mara
huku akipewa support na mzazi mwenzake japo hawako pamoja.

Muigizaji aliyefanya vizuri katika movie kadhaa pamoja na tamthilia ya
Jumba la Dhahabu,
Niva amesema kuwa
hivi sasa ameamua kuingia rasmi kwenye muziki ambao aliwahi kuufanya
kabla hajaingia kwenye uigizaji lakini kipindi hicho muziki ulimtesa
sana akiwa na ndugu yake ambaye waliwahi kufanya wote kazi kwa producer
Enrico.

mwisho kusikika ni katika tukio la kusikitisha lililotokea
siku ya Jumamosi inayohusu familia ya watu sita waliofariki kwa ajali ya
moto Ukonga ambao ni ndugu wa msanii wa
Stereo.
Stereo
amesema taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha moto huo kilisababishwa
na hitilafu ya umeme, watu waliokuwa wakitoa msaada walijaribu
kuwapigia simu Askari wa Zimamoto lakini walichelewa kufika na kushindwa
kutoa msaada wowote, mazishi ya wanafamilia hao yatafanyika kesho huko
Ukonga Banana.
No comments:
Post a Comment