Monday, February 9, 2015

SERIKALI YA MISRI YATOA ADHABU KWA ZAMALEK

Serikali ya Misri imetoa adhabu kutokana na machafuko kwenye uwanja wa mpira jana

misriSasa ni dhahiri kwamba mashabiki wa soka Misri kwa mara nyingine watasahau kwa muda ligi kuu ya nchini kwao baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.
Wengi wa waliofariki ni mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatua mabomu ya machozi wakati wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
fan
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa kutumia nguvu bila tiketi, na walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali zilizopo uwanjani hapo zisiharibike.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa soka zaidi ya 70 walipopoteza maisha wakati vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www,.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment