Monday, May 4, 2015

JARIBIO LA KUTAKA KUJIUA LASHINDIKANA , KILICHOFUATIA NI MAJUTO

Alitamani kujua maumivu ya kupigwa risasi yalivyo..haya ndio maamuzi yake!!

gunKesi za watu kujipiga risasi sio ngeni kusikika na mara kwa mara zimekuwa zikitokea sehemu mbalimbali duniani kutokana sababu mbalimbali ambazo hufikiwa na walengwa.
Hii imetokea kule Hispania baada ya jamaa kukaa na kafikiria ni kwa nini asijaribu kujipiga risasi ili kujua maumivu yake yanakuaje…baada ya kupata jibu akachukua maamuzi mazito.
Mwanaume huyo alikimbizwa hospitali baada ya hali yake kuwa mbaya kufuatia kuamua kujipiga riasi ya mguu ili kuona inakuwaje.
Pamoja na maumivu aliyokuwa nayo aliamua kuitupa bastola hiyo ili kufuta ushahidi kabla ya polisi kumfanyia uchunguzi wa kina.
Jamaa huyo alijitetea kwa polisi  kuwa aliamua kufanya kitendo hicho ili kujua mtu anayepigwa risasi huwa anajisikiaje na bado upepelzi unaendelea ili kuweza kufunguliwa mashtaka.
 Yote haya ynakuja kupitia hapa hapa tangakumekuchablog.com

No comments:

Post a Comment