Wednesday, May 13, 2015

KENYA YAWEKA SHERIA KALI ABIRIA KUTOKA LIBERIA

Maamuzi mapya ya Kenya kwa kila abiria anaetokea Liberia.

airport 1Ugonjwa wa Ebola ulikua tishio kubwa na stori inaongelewa sana kwenye vyombo vya habari hata vya kimataifa miezi kadhaa iliyopita ambapo kwenye nchi kadhaa watu wanaotokea Liberia au nchi jirani zenye ugonjwa huo walipata tabu.
Kenya ilikua imepiga stop abiria wote kutokea Liberia kuingia kwenye nchi hiyo ila sasa kwenye maamuzi mapya serikali ya Uhuru imeondoa marufuku ya muda ya kutowaruhusu hao abiria, wameruhusiwa kuingia kuanzia sasa lakini hata hivyo haimaanishi wataingia tu bila kufanywa chochote.
Kila anaeingia kutoka Liberia  na mataifa jirani yenye ugonjwa huo wataendelea kufanyiwa uchunguzi kila wanapotua hadi ugonjwa huo umalizike kabisa.

No comments:

Post a Comment