Tangakumekuchablog, Tanga
Tanga, KOCHA wa timu ya wanawake JKT Queen inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Robarts
Ngolija, amesema siri ya ushindi mnono walioupata wa mabao 3, 1 kutoka Queen Fair ya Playa ya Tanga ni
umakini wa wachezaji wake.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mpambano huo, kocha
huyo alisema wachezaji wake walikuwa makini na kujitambua wanachokifanya
uwanjani.
Alisema walitambua kuwa Fair Play ni timu kali yenye
wachezaji mahiri hivyo wachezaji wake waliuanza mchezo huo kwa umakini na
kuwasoma kila dakika ilivyokuwa ikienda.
“Ushindi ule ni umakini wa wachezaji wangu kwani wakati
tunakuja kucheza tulitambua kuwa tunaenda kupambana na timu ngumu, niliwaona
wachezaji wangu wanauanza mpira kwa kasi bila mimi kuwapa maelekezo hayo”
alisema Ngolija na kuongeza
“Nafikiri wakati wanaingia uwanjani wao wenyewe waliambizana
namna ya mchezo wauanze, na ndio maana magoli yalingia kama mvua na kupelekea
bao la pili wakajifunga” alisema
Aliwapongeza wachezaji wake kwa uchezaji waliouonyesha na
kuwataka ushindi huo kuwa chachu na endelevu ili kufanya vizuri katika mechi
zilizoko mbele yao.
Kwa upande wake kocha msaidizi wa Queen Fair Play ya Tanga,
Mansour Alawi, alisema haamini kilichotokea uwanjani lakini yote anamuachia
Mungu.
Alisema hakuna mchezaji wa kumlaumu na kuona kila mmoja
licheza vizuri zaidi ya mwenzake na kusema kulikuwa na jinamizi ambalo limepita
hivyo kusema anamwachia Mungu.
“Kwa matokeo ya leo namuachia Mungu kwani sina wa kumlaumu
ila niseme kuwa kuna jinamizi limepuliza wachezaji wangu mabao matatu kama mvua
sio kitu ambacho tumekizoea” alisema Alawi
Aliwataka wachezaji wake kusahau matokeo hayo badala yake
kufanya mazoezi kwa bidii yakiwemo ya kukimbia pamoja na kuogelea baharini ili
kuwa na pumzi za kukimbia uwanjani kwa dakika 90 bila kuchoka.
Mwisho
,Kiungo wa JKT Queen, Merry Masatu, akimdhibiti beki wa
Queen Fair Play ya Tanga wakati wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani jana, JKT
Queen ilishinda kwa mabao 3 , 1.
Wachezaji wa Queen Fair Play ya Tanga wakigombea mpira na wachezaji wa JKT Queen wakati wa mchezo ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani jana , JKT walishinda kwa mabao 3, 1.
No comments:
Post a Comment