Monday, January 5, 2015

AENDESHA GARI AKIWA AMELEWA NA KUGONGA UKUTA WA POLISI,UK

Yamemkuta… Ana kesi ya kugonga ukuta wa Kituo cha Polisi!

car-police_photo
Kukamatwa kwa jamaa aliyegonga ukuta wa Kituo cha Polisi akiwa anaendesha gari huenda ilikuwa moja ya kazi ambazo zilikuwa rahisi zaidi kwa Polisi wa kituo cha Frodsham, Uingereza.
Polisi wamesema jamaa huyo alikuwa amelewa, alipata ajali hiyo alipokuwa akitoka na gari yake katika eneo la Parking ambayo iko  jirani na kituo hicho, akapoteza mwelekeo na kugonga ukuta wa kituo hicho.
Polisi walimkamata na kugundua amelewa, akapandishwa kizimbani kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Hakuna aliyeumia wala kujeruhiwa, ila gari na sehemu ya ukuta wa kituo hicho havikuwa na hali nzuri.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment