Monday, January 12, 2015

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO NA MAGAZETI YA LEO, TZ



Mkusanyiko wa Story kubwa zilizoandikwa na Magazeti ya leo Tanzania January 12, 2015

lineMTANZANIA
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanza kukusanya kodi kwa wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza kama sehemu ya kuongeza mapato yake.
Kwa mujibu wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC wanawake wanaotozwa kodi hiyo ni wale wanaofanya ukahaba katika maeneo ya Manzese, Uwanja wa Fisi sambamba na wanaouza pombe haramu ya Gongo.
Hata hivyo kamati ya Bunge imepinga hatua ya baadhi ya watendaji wa Manispaa hiyo wanaokwenda katika eneo hilo kwa ajili ya kukusanya kodi kwa wanawake hao,kwani kufanya hivyo ni makosa.
Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbaruk alisema kutoza kodi hiyo ni sawa na kuhalalisha biashara hiyo haramu.
Kamati yangu imepata taarifa ya kwambabaadhi ya watendaji wenu wanakwenda Uwanja wa Fisi kukusanya kodi kwa machangudoa,tunajua ukweli kuhusu suala hili hakuna cha kuficha,” alisema Mbaruk.
MTANZANIA
Zaidi ya wanafunzi 300 wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Igovu, iliyopo Mpwapwa, Dodoma wanakaa chini madarasani kutokana na uhaba wa madawati.
Mkuu wa shule hiyo Lwimbo Waziri alisema  mazingira hayo ndiyo yaliyozoeleka shuleni hapo mpaka sasa.
“Hapa tunakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na pia tuna tatizo la uhaba wa madawati hali hii pia inachangai utoro mkubwa kwa wanafunzi,”alisema Waziri.
Mbali na changamoto hizo mwalimu mkuu huyo alisema wanakabiliwa na uhaba wa matundu ya vyoo na kusema ina matundu mawili tu shule nzima ambayo hayaendani na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo.
NIPASHE
Rais Jakaya Kikwete amewaangukia viongozi wa dini akiwaomba kusaidia kudhibiti makundi ya viongozi wanaowania urais walioanza mbio za kujipitisha kwenye nyumba za ibada kunadi sera zao ili kujisafisha njia ya kueleka Ikulu.
Alisema iwapo viongozi wa dini watakataa kuhadaiwa na wanasiasa hao ili  wawape nafasi ya kujitengenezea  kete ya kisiasa ya kutekeleza dhamira zao kupitia nyumba za ibada, watalisaidia Taifa kupata kiongozi mzalendo na mwadilifu.
Alisema katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba,kuwaruhusu wanasiasa kunadi sera zao ndani ya nyumba za ibada ni kuruhusu matatizo.
Rai yangu kwenu viongozi wa dini Muheshimiwa baba askofu,msiwakaribishe tena wanasiasa kutumia maneno ya kanisa kwa shughuliza kisiasa,na ninyi wanasiasa acheni kuchanganya dini na masuala ya kisiasa” alisema Rais Kikwete.
NIPASHE
Shirika la nyumba la Taifa NHC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jijini Arusha,wanatarajia kujenga nyumba za kisasa 4,500 Wilayani Arumeru na Arusha Mjini kuanzia mwezi March mwaka huu.
Meneja wa NHC, James Kisarika alisema wamejiwekea mkakati huo wa kuanzisha mji mpya ujulikanao kama Safari Satelite City katika Wilaya hizo.
Alisema katika ujenzi huo wa nyumba kutakuwepo na nyumba za gharama nafuu 520, kati ya hizo 300 zitaanza kujengwa mwezi March.
Alisema nyumba hizo za gharama nafuu zitamwezesha mwananchi wa kipato cha chini kuishi na kuongeza kiwango cha ajira kwa vijana.
NIPASHE
Baada ya kutangaza kumtema katika kikosi chao cha ligi kuu Tanzania bara, uongozi wa Yanga umesema kwamba utamshtaki aliyekuwa kipa wao Juma Kaseja katika kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka Tanzania, TFF.
Ofisa habari wa Yanga, Jerry Muro alisema  kutangaza kumtema ilikua ni jambo la kwanza na kinachofuata kwa sasa ni kumshtaki kipa huyo katika kamati hizo zinazosimamia soka la Tanzania.
Alisema pia Yanga imepanga kumshtaki Kaseja katika mahakama za kawaida za nchi kwa sababu kuna baadhi ya makosa aliyoyafanya hayahusiani na soka peke yake.
Tunajipanga kuandaa malalamiko kwenda katika kamati za nidhamu na sheria  na haki za wachezaji, hatutaishia kumtema tu“, alisema Muro.
MWANANCHI
Mtu mmoja anashikiliwa na Polisi Mjini Korogwe baada ya basi la Kilimanjaro kukamatwa katika kizuizi cha Polisi eneo la Chekelei likiwa na shehena inayodaiwa kuwa ya milipuko.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraizer Kashai alisema aliyeshikiliwa ni kondakta wa basi hilo ambalo liliruhusiwa kuendelea na safari na kwamba mwenye mzigo huo alikamatwa Arusha  na taratibu za kumfikisha Korogwe zilikua zikiendelea.
Kamanda huyo hakutaka kueleza kwa kina aina ya milipuko hiyo na kusema watafanya hivyo leo.
MWANANCHI
Askofu mpya wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dk. Fredrick Shoo jana alitoa ujumbe mzito kwa Rais Jakaya Kikwete akimtaka kuwawajibisha haraka wahusika wa kwenye kashfa ya Escrow kwa kuwa ‘viporo vinaumiza tumbo’.
Alisema kanisa linasikitishwa na ufisadi mkubwa unaoendelea kwa viongozi wa umma na kiburi wanachokionyesha wanapoambiwa ukweli.
Mimi sioni mantiki kama mtu amehusika katika mambo fulani halafu anaanza kusema sikueleweka vizuri alafu anajiuzulu,tunatambua Rais ameanza ameanza kuchukua hatua kwa watu kama hawa, tunamwombea yeye na Serikali yetu kuchukua hatua zaidi zinazofaa kuchukuliwa” –Shoo.
Panapohitajika kuchukua hatua tusiweke kiporo, unajua viporo vikishakua vya muda mrefu vinaumiza tumbo”, alisisitiza Askofu huyo.
HABARILEO
Watu saba wanahofiwa kufa maji na wengine 49 wameokolewa kutokana na boti waliyokua wkaisafiria kukumbwa na dhoruba katika eneo la vijiji vua mwambao wa Kusini mwa Ziwa Tanganyika.
Kamanda wa Polisi Kigoma, Jafar Mohamed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema boti ya mizigo  ambayo ilikua imebeba watu zaidi ya 50 ilikua ikitokea  nchini Burundi.
Taarifa ya kamandawa Polisi inapingana na taarifa iliyotolewa awali na wananchi waliozungumza na waandishi wa habari  katika eneo la tukio.
Watu hao walisema watu saba wanahofiwa kufa wakati polisi wakiileza kuwepo na taarifa ya kifo cha mtu mmoja.
Kamanda Jafar alisema boti hiyo ilikumbwa na dhoruba kati ya vijiji vya Sigunga na Herembe majira ya saa nane usiku na saa kumi alfajiri.
Alisema kabla ya kukumbwa na dhoruba hiyo na kuzama, abiria wakisaidiana na wafanyakazi wa boti hiyo walijaribu kutosa majini mizigo mbalimbali iliyokuwemo kwenye boti lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,kumekuchablog

No comments:

Post a Comment