
Serikali
ya Tanzania inatarajiwa kuingilia kati kuhusiana na marafuku iliowekewa
magari ya Utalii ya taifa hilo yanayosafirisha watalii kati ya Arusha na
Nairobi kutoingia katika uwanja wa Ndege wa JKIA jijini Nairobi.
Wahudumu
wa magari hayo waligoma kwa masaa kadhaa wakingojea msimamo wa serikali
kuhusu marufuku hiyo iliowekewa magari hayo ya Tanzania mnamo mwezi
Disemba mwaka jana.
Kulingana
na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Waziri wa mali asli na utalii
Lazoro Nyalandu amewahakikishia wahudumu hao kwamba atasafiri hadi
jijini Nairobi pamoja na wawakilishi wao ili kuzungumza kuhusu swala
hilo na mwenzake wa Kenya.
''Serikali
yetu pia imeshangazwa na hatua hiyo ya Kenya kwa sababu viwanja vya
ndege havihusiki katika makubaliano yalioafikiwa na mataifa hayo
jirani'',alisema.
Mbuga ya
wanayama pori Nyalandu amekiri kwamba Tanzania mwaka 1985
iliafikiana na kenya kupiga marufuku magari ya kenya ya Utalii kutoingia
katika mbunga zake za wanayama pori,hatua ambayo ililenga kuwawezesha
wahudumu wa magari ya Utalii ya nchini humo.
''Marufuku
hiyo ya Kenya inamaanisha uwanja huo wa ndege sasa ni kivutio cha
watalii badala ya eneo la kuingilia Kenya'',alishangaa Nyalandu akisema
hatua hiyo imewagharimu wahudumu wa utalii nchini Tanzania.
Lakini
wachanganuzi wanaamini kwamba marufuku hiyo ya Kenya ni hatua ya
kulipiza kisasi dhidi ya hatua ya tanzania kufunga mpaka wa Bolongoja
uliopo kati ya mbuga ya wanayama pori ya Serengeti na masai Mara ya
Kenya miaka ya 70.
No comments:
Post a Comment