Sunday, January 11, 2015

UKUBWA NA UBWANYENYE WAMPONZA WAZIRI ,UTURUKI

Boss alibebwa na wakulima ili viatu visiharibike kwenye barafu, kilichofuatia ni story!

Snow
Picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii Uturuki zikimuonyesha kiongozi wa Idara ya Huduma Vijijini akiwa amebebwa juu na wakulima ili kukwepa barafu zilimponza, ikaamriwa asimamishwe kazi.
Afisa huyo, Nedim Zunarci alionekana amebebwa na wakulima hao katika Jimbo la Manisa wakati akikagua athari zilizosababishwa na barafu aliyoanguka kutokana na baridi kali, akahofia viatu vyake vitaharibika kutokana na barafu hiyo, hivyo akabebwa na wakulima hao.
Meya wa Manisa, Cengiz Ergun alisema kitendo hicho hakiendani na utaratibu wa kazi wala maadili, pia hakionyeshi uhusiano mzuri kati ya viongozi na jamii.
Comments za watu kwenye mitandao ya kijamii Uturuki walionekana kukosoa pia kitendo hicho baada ya picha hiyo kuzagaa.
Unahitaji kupata kila stori inayonifikia mtu wangu? Ni rahisi sana, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekuchablog

No comments:

Post a Comment