Hii ni Hekaheka ya leo Feb 9 inatokea Dar; inahusu msiba ulioleta mvutano.

Ndugu mmoja wa marehemu amesema kuwa
ndugu yao alikuwa anaumwa ugonjwa ambao hawakuujua, mume wake ndio
alikuwa karibu naye akimuuguza mpaka alipofariki kitu ambacho kilifanya
ndugu kuhusiisha kifo hicho hicho na imani za kishirikina.
Ndugu hao wamesema kuwa wanachotaka ni
kushiriki mazishi ya ndugu yao lakini mume huyo alikataa ndugu yoyote
kushiriki kwenye jambo lolote kwenye msiba huo ikapelekea suala hilo
kufikishwa Mahakamani lakini baadae walikaa na kukubaliana kufanya
mazishi Dar.
Mume huyo amesema kuwa mke wake
alipokuwa anaumwa hakupata msaada wowote kutoka kwa ndugu japokuwa
walikuwa na taarifa juu ya kuumwa kwa mke wake.
No comments:
Post a Comment