Tuesday, March 14, 2017

MAHARAMIA WATEKA MELI YA MIZIGO PWANI YA SOMALIA

Maharamia wa Somalia katika pwani ya taifa hilo wanadaiwa kuiteka nyara meli ya mizigo ya Sri-LankaMeli moja ya mizigo imetekwa nyara katika pwani ya Somalia kulingana na ripoti.
Baadhi ya maharamia hao walipanda meli hiyo yenye bendera ya Sri-Lanka katika pwani ya kaskazini ya taifa hilo siku ya Jumatatu kulingana na wakaazi na maafisa.
Msemaji wa jeshi la wanamaji wa muungano wa bara Ulaya linaloendesha operesheni zake dhidi ya maharamia katika eneo hilo amesema kuwa ni mapema mno kuthibtisha utekaji huo.
Iwapo itathibitishwa ,utakuwa utekaji nyara wa kwanza wa meli ya kibiashara na maharamia wa Somalia tangu 2012.
Wanamaji wa muungano wa Ulaya waliambia BBC : Tumegundua kuhusu hili Jumatatu jioni na ndege imetumwa katika eneo hilo kuchunguza.
John Steed wa kundi la misaada la Oceans Beyond Piracy akizungumza na Reuters alisema ,meli hiyo iliripoti kwamba ilikua ikifuatwa na boti mbii jana jioni baadaye ikapotea.

No comments:

Post a Comment