Monday, March 20, 2017

I PHONE NI MAMBO YOTE

Siri katika iphoneWatu wenye kufanyia wengine mzaha wamekuwa wakiwahadaa wanaotumia simu za iPhone kutamka 108 kwenye huduma ya kutambua sauti ya Siri.
Bila kujua, wamekuwa wakihadaiwa kupiga simu kwa polisi na huduma za dharura.
108 ni sawa na 999 nchini India, hivyo Siri inafasiri hatua hiyo kama jaribio la anayetumia simu kupiga simu ya dharura.
Na hivyo, hilo linaifanya kupiga mara moja simu ya dharura hadi kwa polisi au maafisa wa huduma za dharura.
Kufanyia mzaha watu sana huwa hakuna madhara, lakini katika hili wanawafanya watu kupotezea muda maafisa wa kushughulikia dharura.
Usipojihadhari, katika nchi nyingi kuna sheria inayotoa adhabu kwa watu wanaopotezea muda maafisa wa dharura kwa kupiga simu bila kuwa na tukio lolote la kupiga ripoti.
Kuna wengine wanaozidi katika utani huu, kwa kuwashauri wenye simu "kufunga macho sekunde tano" wanaposoma 108.

No comments:

Post a Comment