KOROGWE, NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo, amemuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Korogwe, Robarts Gabriel, kuhakikisha Mkandarasi ujenzi wa stendi
mpya ya Kilole anakamilisha mwishoni mwa mwezi huu vyenginevyo akatwe pesa na
kunyimwa tenda Wilayani humo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa stendi hiyo inayojengwa na kampuni
ya Namis Coperate Contractor ambayo
iliomba kuongezewa muda, Jafo alisema lazima ujenzi huo ukamilike ndani ya
mwezi huu.
Alisema stendi hiyo ilitakiwa kuanza kutumika kwa mabasi
yaendayo Mikoani na Wilayani hivyo kutaka ikamilike kabla ya mwezi huu kuisha.
“Mkuu wa wilaya nakuagiza stendi hii kama haitakamilika
mwisho wa mwezi huu mkandarasi akatwe pesa na kunyima tenda zote za halmashauri
yako” alisema Jafo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Korogwe, Robarts Gabriel
aliwataka wafanyabiashara na wasafirishaji kuitumia stendi hiyo mara baada
kukamilka kwa uchumi wa Wilaya hiyo.
Alisema stendi hiyo ambayo mabasi yote yaendayo Mikoani na
Wilayani yatakuwa yakiingia hivyo kuwataka wafanyabiashara kuwekeza katika
miradi mbalimbali ya kibiashara.
Nae Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stivin Ngonyani,
aliwataka wajasiriamali wadogowadogo wakiwemo wa kazi za mikono wataweza
kujitangaza na kuuza bidhaa zao tofauti na stendi ya zamani ambayo ilikuwa
finyu.
Alisema kukamilika kwa stendi hiyo kutaweza kuinua kipato cha
wajasiriamali wadogowadogo hivyo kuwataka kujiimarisha katika kazi zao.
‘Ujio wa stendi mpya ni neema kwa wajasiriamali wadogowadogo
hasa wa kazi za mikono kwani mabasi yote yaendayo na yatokayo mikoani yataingia
stendi hiyo ambayo itakuwa ya kisasa” alisema Majimarefu
Aliwataka wananchi wa Korogwe kuipokea stendi hiyo kwa kubuni
biashara ambazo zitaweza kuwabadilisha kimaisha kwa kuenua vipato vyao.
No comments:
Post a Comment