![Magunia yaliyokuwa na pesa](http://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/51E5/production/_95156902_c32891cd-6020-4221-859c-6d70173e61e4.jpg)
Maafisa wa serikali nchini Nigeria
wanasema magunia matano yaliyokuwa na mabunda ya noti yamegunduliwa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.
Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege.
Fedha
hizo, za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa
wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.
BBC
No comments:
Post a Comment