Thursday, March 23, 2017

NYOKA AGUNDULIKA NDANI YA NDEGE IKIWA ANGANI

NyokaNyoka amegunduliwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kuelekea mji wa Anchorage katika jimbo la Alaska Marekani.
Taarifa zinasema nyoka huyo aliachwa kwenye ndege hiyo na abiria.
Alikuwa ameorodheshwa kama 'mnyama kipenzi' na abiria huyo katika safari nyingine iliyokuwa imefanywa na ndege hiyo.
Abiria walifahamishwa kuhusu uwepo wa nyoka huyo rubani alipotangaza: "Jamaa, tuna nyoka ndani ya ndege hii, lakini hatujafahamu yuko wapi hasa."
Nyoka huyo wa futi tano hakuwa na sumu na alionekana mara ya kwanza kwenye ndege na mvulana alikuwa amepanda na kusimama juu ya kiti.
BBC

No comments:

Post a Comment