Mwanamke wa Misri anayeaminiwa kuwa
mwenye uzito wa juu zaidi duniani akiwa na kilo 500, amefanyiwa
upasuaji wa kupunguza unene chini India." Tunajaribu kumuwezesha kuwa mwenye nguvu za mwili kuweza kusafiri nyumbani Misri haraka iwezekanavyo," ilieleza taarifa ya hospitali.
Familia yake ilisema kuwa hajawahi kuondoka nyumbani kwao kwa miaka 25 hadi siku aliposafirishwa hadi India mwezi Januari kwa ndege.
No comments:
Post a Comment