![Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubaraka ameachiliwa huru baada ya kuhudumia kifungo cha miaka kadhaa](http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/BA54/production/_95300774_hosnimubarak.jpg)
Aliyekuwa rais wa Misri Hosni
Mubarak ameripotiwa kuachiliwa huru baada ya kuhudumia miaka jela
kufuatia maandamano yaliomng'atuwa mamlakani 2011.
Mubarak
alikuwa akizuiliwa katika hospitali ya kijeshi mjini Cairo, lakini
wakili wake aliiambia BBC kwamba sasa ameruhusiwa kurudi nyumbani kwake
mjini humo.
Aliagizwa kuachiliwa huru mapema mwezi huu baada ya
mahakama ya rufaa kumuondolea makosa ya kuwaua waandamanaji wakati wa
maandamano dhidi yake 2011.
No comments:
Post a Comment