Thursday, March 16, 2017

RASHFORD AITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA ENGLAND

Marcus RashfordMshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford atatajwa kwenye kikosi cha meneja wa England , Gareth Southgate siku ya Alhamisi.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 hapo awali alitarajiwa kushirikishwa katika upande wa vijana mwenye chini ya umri wa miaka 21 watapokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Denmark wikendi ijayo.
Lakini na washambuliaji wa England HarrRy Kane na Wayne Rooney wote wametolewa kutokana na majeraha , huko Rashford akitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.
England itakabiliana na Ujerumani katika mechi ya kirafiki kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania huko Wembley tarehe 26 mwezi Machi .

No comments:

Post a Comment