Tanga, JESHI la polisi, Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi vimekamata
shehena za mali ya magendo katika bandari bubu ya Kigombe.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ghala la kuhifadhia
mali jana, Menaja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, Swalehe
Byarugaba, alisema shehena hizo ni pamoja na mchele, sukari, madumu ya mafuta
na viberiti kutoka nje vyenye thamani zaidi ya milioni 73.
Alisema kwa wiki nzima wamekuwa wakifanya doria hasa vyakati
za usiku katika bandari bubu ya Kigombe na sehemu nyengine ambazo wamekuwa
wakipokea taarifa za ushushaji wa mali za magendo.
“Kama munavyoona humu hizi zote ni mali za magendo ambazo
tumekuwa tukifanya doria katika bandari zetu na kufanikiwa kukamata na zote
zikiwa ni kutoka nje” alisema Byarugaba
Alisema katika mali hizo manahoza wa vyombo wamevitekeleza
vyombo vyao na wengine kufanikiwa kuwakamata na kuwachia vyombo vya usalama kwa
hatua za kisheria.
Akizungumza kwenye uonyeshaji wa mali hizo za magendo,
kamanda wa polisi Tanga, Benedickti Wakulyamba, alisema kikosi chake kwa
kushirikia na vyombo vyengine vya ulinzi wamekuwa wakifanya doria usiku na
mchana bandarini na mpakani horohoro.
Alisema kuna baadhi ya washukiwa wa mali za magendo wamekuw
wakihojiwa na wengine kufuatilia na kutoa onyo kwa wasafirishaji wa mali za
magendo kuwa wametangaza vita.
Alisema doria hiyo itakuwa endelevu usiku na mchana hivyo
kufuatilia nyendo za watu ambao wamekuwa wakiwahisi kujihusisha na biashara ya
haramu ikiwemo mali za magendo.
“Natangaza vita kwa wasafirishaji wa mali za magwendo na
wapitishaji wa madawa ya kulevya kuwa hakuna mlango wakupitishia, na yoyote
ambaye atajaribu cha mtema kuni atakiona” alisema Wakulyamba
Alisema jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wa madawa ya
kulevya ikiwemo mihadarati na wasafirishaji wa mali za megendo na uchunguzi
ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga,
Swalehe Byarugaba (kushoto) na Kaimu Meneja msaidizi Forodha Tanga, Jumbe
Magoti wakiangalia nembo ya moja ya mifuko 1,308 ya mchele kutoka nje
iliyokamatwa katika bandari bubu ya Kigombe wakati wa operesheni iliyofanywa
wiki nzima kwa kushirikiana na jeshi la polisi, TRA, wavuvi na vyombo vya
usalama na kukamata bidhaa mbalimbali zenye thamani zaidi ya shilingi milioni
73.
No comments:
Post a Comment