Monday, March 20, 2017

MBUNGE JIMBO LA TANGA MJINI, MUSSA MBAROUK AFANYA ZIARA HOSPITALI ZA TANGA MJINI



 Mganga Mfawidhi hospitali ya Makorora Tanga, Saleh Mayenjo, akimuonyesha Mbunge wa jimbo la Tanga mjini (CUF) Mussa Mbarouk ufa wa ukuta ndani ya wodi ya wazazi wakati alipofanya ziara kuona changamoto na kutoa msaada wa mashuka na chandarua kwa wodi ya wajazito jana.
Mbunge huyo mbali ya kujionea changamoto nyingi katika hospitali hizo ikiwemo ya Ngamiani na Makorora pia litoa msaada wa mashuka na vyandarua kwa wagonjwa waliolala hospitalini hapo na kuongeza chachu ya kazi ya Serikali katika kupambana na Malaria nchini.



 Mganga Mfawidi hospitali ya Makorora Tanga, Saleh Mayenjo akimuonyesha Mbunge wa jimbo la Tanga mjini (CUF) Mussa Mbarouk ufa ukuta wa wodi ya mama wajazito wakati alipofanya ziara kujionea changamoto inazoikabili hospitali hiyo na kutoa msaada wa mashuka na vyandarua wodi ya wanawake jana.


No comments:

Post a Comment