Thiery Henry kumrithi Wenger
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry (39) huenda akarithi
mikoba ya Arsene Wenger anayemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaj huyo aliyeacha jina kwenye klabu yake hiyo ya zamani, hata hivyo
amesema hana uhakika iwapo ndiye atakarithi mikoba hiyo ya bosi wake
wa zamani ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na presha ya
kutakiwa kuondoka klabuni hapo.
Mkabata wa Wenger unaelekea ukingoni mwishoni mwa masimu huu na mpaka
sasa hajui hatima yake klabuni hapo kutokana na kuwapo mvutano iwapo
abaki au aendelee kukinoa kikosi hicho.
Msukumo mkuwa wa kutakiwa kuondoka ulishinikizwa na mashabiki wa timu
hiyo baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Europa, huku
wakimpa presha kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa katika nafasi za juu
kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
No comments:
Post a Comment