Monday, March 27, 2017

WASICHANA WALIOKUWA WAMEVALIA SURUALI YA KUBANA WAZUIWA KUPANDA NDEGE

Ndege za United AirlinesShirika la ndege la United Airlines nchini Marekani limeshutumiwa sana baada ya kudaiwa kuwazuiwa wasichana wawili waliokuwa wamevalia suruali ndefu za kubana kuabiri ndege hiyo.
Kisa hicho kilitokea kwenye safari ya ndege iliyokuwa ikitokea Denver kuelekea Minneapolis Jumapili asubuhi, mwanaharakati Shannon Watts amesema.
Shirika la United limesema wasichana hao walikuwa wanasafiria hati maalum, ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa shirika la ndege na wageni wao.
United wamesema huwa kuna kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo kusafiria.
Shirika hilo limefafanua kwamba abiria wa kawaida, ambao wanalipia tiketi zao, wako huru kuvalia mavazi yao ya kubana.
BBC

No comments:

Post a Comment