Friday, March 24, 2017

WAZIRI NCHEMBA AAGIZA ALIECHOMOA BASTOLA KUADHIBIWA

Waziri ashutumu askari kwa kuchomoa bastola wakimdhibiti Nnauye

Bw Nchemba akiwa na Rais MagufuliWaziri wa mambo ya ndani nchini  Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari  kuchomoa bastola na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.
Nchemba, (Pichani kushoto) na Rais Magufuli (kulia) kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika.
BBC

No comments:

Post a Comment