Hapa Tanzania, Uganda , Rwanda na
hata Burundi na Kenya utaona mabango makubwa yamewekwa kando ya barabara kuonya
madereva kuto endesha magari wakiwa wamelewa .Lakini nchini Taiwan mambo ni tofauti kabisa.
Dereva yeyote anayepatikana na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi , anakamatwa na kupelekwa kwenda kufanya kazi katika chumba cha kuhifahdi maiti.
Mkuu wa mashtaka katika jimbo la Taitung huko Taiwan, ameiambia BBC kwamba madereva wanaopatikana na kosa la kuendesha gari wakiwa wamelewa wanapewa kazi maalum ya kusafisha meza za kuwa pasulia maiti. Na pia wanatakina kuosha na kusafisha kabisa friji za kuwekea maiti.
No comments:
Post a Comment