Monday, March 27, 2017

NAY WA MITEGO ACHIWA HURU

Wa Mitego baada ya kuachiliwa huruMwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi Tanzania kuhusiana na wimbo wake, ameachiliwa huru.
Wa Mitego ameachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru.
"Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhuru wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu," amesema Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru.
Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: "Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote."
Dkt Mwakyembe hata hivyo alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.
BBC

No comments:

Post a Comment