Saturday, March 11, 2017

RC, SHIGHELLA NA NUNDU WAIPONGEZA TTCL TANGA KUANZISHA 4G TANGA



Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, ameipongeza kampuni ya simu Tanzania (TTCL) kuanzisha huduma mpya ya 4G LTE na kusema kuwa kampuni hiyo imeuwasha moto kama ilivyokuwa zamani.
Akizindua huduma mpya za 4G LTE, juzi, Shigella, alisema kampuni hiyo imewakonga nyoyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake mbali ya unafuu tofauti na mitandao mengine pia utoaji wa simu utawavutia wengi.
Alisema ulimwengu huu wa utandawazi watu wengi hukimbilia kuliko na mawasiliano nafuu jambo ambalo wateja wengi wanaweza kukimbilia  TTCL ambako linawezekana.
“Huduma hii mpya ya simu ya mkononi yenye nguvu inaweza kuongeza chachu ya ushindani wakibiashara hasa kwenu upande wa mawasiliano, nawaomba unafuu uliopo uongezeni uwe nafuu zaidi” alisema Shigella
Aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kuongeza nguvu na moyo wa utendaji kazi na kuwa wabunifu kwa kuelewa kuwa kampuni hiyo ndio baba na mama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Omari Nundu, aliwataka Watanzania kuwa na ada ya kupenda bidhaa zao ili faida inayopatikana ibaki mikononi mwao.
Alisema Kampuni hiyo mbali ya changamoto ambazo inalikabili atahakikisha linarudi katika makali yake ya zamani na kuwa washindani wa kweli.
“Tuwe na ada ya kupenda cha kwetu ili faida ipatikanayo iendelee kubaki mikononi mwetu, leo tumezindua huduma hii ambayo ni mwanzo ila tambueni kuwa mwendo kasi umeanza” alisema Nundu
Nae Afisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba, amevitaka vyombo vya usalama na ulinzi kuilinda miundombinu ya kampuni hiyo ambayo hufanyiwa hujuma mara kwa mara.
Alisema kuna baadhi ya wahalifu wamekuwa wakiihujumu miundombinu ya kampuni hiyo na kurudisha nyuma jitihada za kuwaletea wananchi huduma ya mawasiliano.



, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, akizungumza wa watendaji, wafanyakazi wa watumiaji wa simu ya TTCL wakati wa uzinduzi wa huduma za simu ya mkononi ya  4GLTE katika ofisi za kampuni hiyo Tanga juzi.


Mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya Simu Tanzania, Omari Nundu, akizungumza na wafanyakazi, wageni na watumiaji wa simu ya TTCL wakati wa uzinduzi wa huduma za simu ya mkononi ya  4G LTE katika ofisi za kampuni hiyo Tanga juzi.

No comments:

Post a Comment