Irene Uwoya - Macho mbele nje ya nchi

Katika
kile kinachoonekana waigizaji wa kike kutaka kukuza tasnia ya uigizaji
kwa kuvuka mipaka ya nchi, mwigizaji Irene Uwoya amesema kuwa anataka
atambulike nje ya nchi kuliko ndani.
Akiweka
hoja yake sawa, mwanadada huyo anayedaiwa kuendelea kuwa na mvuto katika
tasnia ya filamu alisema anajua kuwa siyo jambo rahisi kufanya vizuri
nje ya nchi, lakini huko ndiko anakotaka kufika, hivyo anyeshe mvua au
liwake jua, atajitahidi kuhakikisha kwamba ndoto zake zinatimia.
Uwoya
alisema kuwa alijaribu kutengeneza mtandao wa kazi na wasanii wa nje
wakati anatayarisha filamu ya 'Kisoda' ambayo picha zake zilipigwa
nchini Afrika Kusini na Uturuki. Alifafanua kama wakati mwingine siyo
lazima kusafiri, kuna wakati wasanii wa nje wanaweza kuja Tanzania
kikazi, ujio wao ni nafasi ya pekee kwao, au kwa kufanya nao kazi
hapahapa, ama kuchukua mawasiliano na kuwafuata baadaye kwa ajili ya
kufanya nao kazi.
"Tena
nawaambia wale wote wenye nafasi au wanaofahamiana na watu wanaopenda
kwa dhati kufanya kazi na waigizaji wa Tanzania, wasikose kuwaambia hata
mimi napenda na ninaweza kufanya hivyo, "alisema Uwoya.
Mwigizaji
huyo alifafanua kuwa njia pekee ya kutangaza kazi za ndani Kimataifa ni
kufanya kazi na waigizaji wa nchi nyingine ambao watakuwa na hamu ya
kukufuatilia na kufuatilia kazi zetu nyingine pia. Aliongeza kuwa kwenye
muziki angalau kuna mwanga, lakini kwenye uigizaji bado juhudi
inahitajika kwani baada ya kufariki dunia kwa mwigizaji Steven Kanumba,
mbio za kujitangaza kama zimefifia.
Kauli
hiyo ya Uwoya imekuja wakati waigizaji kadhaa wakionyesha nia kama yake
akiwamo Wastara anayenadi filamu mpya ya 'Mateso wanayopata Watanzania
nje ya nchi' na mwigizaji anayedaiwa kuwa na nguvu ya kukubalika kwenye
jamii Wema Sepetu akiwa amerudi juzi kutoka nchini Ghana ambako
alikwenda kupiga picha za filamu yake iitwayo 'After Death'Yote kupitia kumekuchablog
No comments:
Post a Comment