Mkusanyiko wa Stori kubwa muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo January 11, 2015
Rais Jakaya Kikwete ametangaza habari njema kwa Watanzania kwamba kuanzia mwaka kesho elimu ya Sekondari na msingi itatolewa bure.
Alisema hatua hiyo inakuja baada ya
kukamilisha sera mpya ya elimu na ufundi ili kuboresha sekta hiyo
ambayo imepitishwa na Baraza la Mawaziri.
Hatua hiyo inachukuliwa katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata kiwango hicho cha Elimu kwa gharama inayobebwa na Serikali.
“Kwenye
sera mpya,imeanisha jinsi ya utoaji wa elimu bora na viwango
vinavyokubalika katika ufundi,hii itawezesha elimu hizi mbili kukidhi
matakwa katika soko la ajira pamoja na kujiajiri“alisema.
Hatua ya Rais kutangaza azma ya kutoa
elimu bure imekuja miaka 10 baada ya wapinzani hasa Chadema kueleza kuwa
moja ya mikakati yao ni kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania iwapo
watachaguliwa kuongoza nchi.
NIPASHE
Zoezi la kuwaapisha watu 500 wakiwemo
wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa na wa Vitongoji katika
Halmashauri ya mji wa Tarime limekwama kwa mara ya pili.
Hatua hiyo imesababishwa na kutokea
vurugu zinazodaiwa kuwa zinafanywa na wafuasi wa Chadema wanaokataa
kuwapa ushindi wagombea wa CCM wakati kura zilikua na utata.
Wafuasi wa Chadema wapinga kuapishwa kwa
aliyekua mgombea wa CCM Kitongoji cha Highway,baada ya kumnyan’ganya na
kuchana fomu za kiapo na kutaka aapishwe mgombea wa Chadema hali
iliyozusha vurugu.
Katika vurugu hizo watu walirushiana
viti,kukabana,kuvutana mashati hai iliyosababisha ukumbi kuzizima kwa
fujo na kumlazimu hakimu aliyekua afanye kazi hiyo kutowaapisha
wenyeviti hao ambao walipanga kuapishwa juzi baada ya zoezi hilo
kushindikana Desemba 30.
NIPASHE
Polisi aliyetimuliwa kazi,Godfrey Mashumbusi amewakata mapanga na kuwajeruhi vibaya mama na mwanaye kisa wanadaiwa chupa mbili tupu za bia.
Mama huyo na mwanaye ambaye ni
mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam walikatwa mapanga na kupigwa
virungu wakiwa maeneo tofauti katika baa inayojulikana kwa jina la Itawa
inayomilikiwa na askari huyo.
Mkasa huyo ulitokea Tabata
Kisukuru,ulithibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa IlalaMarietha
Minangi ambaye alisema chanzo ni familia hiyo kushindwa kupeleka chupa
hizo kwa wakatib na kulipa deni la shilingi 10,000.
Akielezea tukio hilo mama huyo Sekela
Mwiniwasa alisema alimwagiza mdogo wake bia mbili kwenye baa hiyo na
siku iliyofuata alipita kwenye baa hiyo na kuulizwa kwanini hajarudisha
chupa na alijibu amezisahau nyumbani ndipo akaanza kumshambulia kwa
mapanga kabla ya kumfuata mtoto wake na kumfanyia hivyo hivyo.
NIPASHE
Manispaa ya Kinondoni inakusudia kufanya
msako wa kufuatilia shule za awali maarufu kama chekechea ambazo
hazijasajiliwa na zinazoendeshwa katika mazingira mabovu.
Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo Kikove Takwimu
alisema kuna utitiri wa shule za awali zisizofuata utaratibu wa elimu
hali inayochangia kushusha viwango vya elimu kutokana na elimu hiyo
kutolewa katika mazingira yasiyoridhisha.
“Ukizunguka katika jiji la Dar es salaam
hasa Kinondoni utakuta shule za awali nyingi ambazo haziko kwenye
mazingira ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na
barabara,gereji,baa na wakati mwingine katikati ya nyumba za
watu,”alisema Takwimu.
Alisema kuwa Wizara ya Elimu na mafunzo
ilitoa utaratibu wa kuanzisha shule za awali kuwa mwananchi anayetaka
kuanzisha kituo hicho awe na heka tatu au zaidi ili kujenga
madarasa,vyoo na viwanja vya michezo pamoja na uwepo wa hewa safi.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe mzito
dhidi ya watakaofanya vurugu ama kuvuruga uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwaka huu,akisema watachukuliwa hatua kali.
Kikwete ambaye anamalizia muda wake wa
miaka 10 tangu akabidhiwe nchi mwaka 2005 ametoa kauli hiyo ikiwa ni
wiki chache baada ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa
kutawaliwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria na taratibu na kusababisha
Wakurugenzi sita kutenguliwaajira zao huku wengine watano wakisimamishwa
kupisha uchunguzi.
“Hatua za
kinidhamu zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watu waliovuruga uchaguzi
wa Serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka jana ni ujumbe mzito kuelekea
uchaguzi mkuu unaokuja“alisema Kikwete.
“Tunatuma ujumbe kuwa matukio kama haya hayatavumilika kwenye uchaguzi mkuu ujao”alisema.
MWANANCHI
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA
imetahadharisha uwezekano wa kutokea kwa mafuriko kufuatia mvua kubwa
inayotarajiwa kunyesha kwa kiwango cha zaidi ya milimita 50 katika
maeneo mbalimbali ya nchi.
Mkurugenzi wa TMA Agnes Kijaza
alisema Mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo ni pamoja na Dar es
salaam,Mwanza,Mtwara,Lindi,Mbeya,Iringa,Njombe,Dodoma,Singida,Ruvuma,Pwani
na Morogoro.
Aliwataka wakazi wa maeneo hayo na
Mamlaka zinzohusika na maafa kuchukua tahadhari stahiki ili kupunguza
madhara yanayoweza kutokea.
“Mvua hizo zinatokana na kuimarika kwa
mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya Hindi lililokaribu na
Pwani ya Msumbuji”alisema Agnes.
MTANZANIA
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amesema Tanzania ni mali ya Watanzania wote na hakuna mtu mwenye hatimiliki.
Lowassa alitoa kauli hiyo kwenye ibada
ya kuapishwa kwa mchungaji Solomon Misangwa wa kanisa la KKKT Dayosis ya
Kaskazini na kati kuwa askofu.
Bila kufafanua kauli hiyo Lowassa ambaye
ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM aliliomba kanisa kuendelea kuombea
amani na utulivu kwa sababu wana wajibu huo na wafanye hivyo wakitambua
Tanzania ni ya Watanzania wote.
Alisema kanisa lina wajibu wa kuendelea
kusaidia miradi mbalimbali linayoiendesha,lakini pia halipaswi kuacha
kuiombea nchi amani huku akikumbusha msuguano uliotokea kati ya
wajumbewa Bunge la Katiba wakati lilipokua likiketi kuandika katiba
inayopendekezwa.
MTANZANIA
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Janeth Mbene,
amejitosa katika sakata la sukari za magendo na kulitaka Jeshi la
Polisi kufanya doria maeneo ya mipakani ili kulinda viwanda vya ndani.
Mbena alisema suala hilo ni dogo katika
kulinda viwanda vya ndani na kaahidi kushirikiana na Mamlaka husika ili
kuhakikisha wanaoingiza sukari hiyo wanadhibitiwa.
“Ni jambo
la aibu kwa baadhi ya Watanzania kuendelea kuingiza sukari kwa njia ya
magendo nchini huku viwanda vya ndani vikipoteza soko,pia ajira nyingi
za Watanzania zipo shakani katika viwanda vya sukari vya ndani kwa
kiwango kikubwa“alisema Mbene.
Alisema uingizwaji wa sukari ya magendo
kutoka nje ya nchi unakera kwa kuwa tunasaidia kutengeneza ajira za watu
wa nchi za nje huku Watanzania wenzetu wakikosa ajira na kupunguzwa
kazini kutokana na kile wanachokizalisha kutofika kwa mlaji moja kwa
moja.
Alitaja miongoni mwa njia watakazotumia
kukamata sukari inayoonekana imeingizwa nchini kinyume na utaratibu ni
kuwatumia askari,TRA kupitia doria endelevu na kufanya ukaguzi katika
maduka makubwa.
JAMBOLEO
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ
litaendelea kutumika endapo litahitajika sehemu yoyote duniani kwa
ajili ya kusaidia kulinda amani ya watu ambao wamekua wakipoteza maisha
bila hatia kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha Jeshi hilo litaendeleza mapambano
dhidi ya waasi wanaopigana na majeshi ya Serikali ya Congo,Mashariki mwa
nchi hiyo ili kuyatokomeza kabisa na kutoendelea kuleta madhara kwa
nchi jirani.
Rais Jakaya Kikwete alisema hadi sasa
Tanzania imetoa wanajeshi 3,000 kwenda UN ili kuendelea kulinda amani
Congo,Durfur na Lebanon na Tanzania imekua nchi ya sita kuchagia jeshi
kwa lengo la kulinda amani Afrika.
Kwa upande wa duniani JK alisema
inashika nafasi ya 12 na kuheshimika barani Afrika na duniani kote hivyo
sera ya mambo ya nje ni kuendeleza yale yote mazuri yaliyofanywa kwa
ajili ya kutaka bara la Afrika na duniani watu waishi kwa amani.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekuchablog
No comments:
Post a Comment