Kizaazaa cha Askari wa Ufilipino kuvaa pampers wakati wa ziara ya Papa Francis…

Siku chache zilizopita kulikuwa na
taarifa kwamba kuna ugeni wa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ambapo
atakuwa anatembelea Ufilipino.
Ambacho sikuwa nimejua ni hii kuhusu taarifa ya agizo rasmi kwa matrafiki na maofisa usalama wa Ufilipino kutakiwa kuvaa pampers
muda wote wakati wa ziara ya Papa ambayo itakuwa kati ya tarehe 15-19
January, hilo lilikuwa agizo la Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya
Metropolitan Manila, Francis Tolentino.
Lengo la agizo hili ni kuwafanya Askari na maafisa hao kuwa kazini muda wote wakati wa ziara ya Kiongozi huyo.
Ziadi ya trafiki 2,000 ambao watakua
kazini katika ziara hiyo itakayoanza Januari 15 hadi 19 watatakiwa kuvaa
nepi hizo zitakazowawezesha kukaa katika maeneo yao ya kazi bila
kuondoka kwenda kujisaidia wakati wa ziara ya Papa.

Ofisa wa Mamlaka ya Maendeleo ya Metropolitan Manila, Emerson Carlos alisema nepi hizo zitafanyiwa majaribio wakati wa maandamano maalum ya Black Nazarene.
“Tutawapa
nepi hizi kwa sababu hatufahamu ni wakati gani mkusanyiko wa watu
utaongezeka zaidi, tunataka amani itawale wakati wote wa ziara“– Carlos.
Nchi hiyo inatarajia ugeni mkubwa wa
mamilioni ya watu kutoka Asia kujitokeza kumuona Papa na pia kushiriki
ibada maalum atakayoiongoza tarehe 18 huko Manila.
Unadhani bongo ingekuwa vipi story ya matrafiki kuvalishwa pampers?
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kupitia kumekuchablog
No comments:
Post a Comment