Rais wa Baraza la muungano wa Ulaya
Donald Tusk ameonya kwamba maamuzi ya kutia wasiwasi yanayofanywa na
Donad Trump ni miongoni mwa chanagmoto zinazokumba muungano huo.
Amesema
kuwa mabadiliko yaliofanyika nchini Marekani ni miongoni mwa vitisho
kutoka nje vinavyojumuisha China, Urusi na Waislamu wenye itikadi kali
kwa muungano huo.Katika barua kwa viongozi 27 wa bara Ulaya, Tusk pia amesema kuwa anaamini kwamba wote wanakubaliana naye.
Taarifa kadhaa kutoka Washington zimesababisha maandamano dhidi ya Trump katika miji mikuu ya Ulaya.
BBC
No comments:
Post a Comment