Thursday, March 31, 2016
LICHA JOTO NA JUA KALI, TMA YASEMA MVUA IPO PALE PALE
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa TMA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema maeneo yaliyotolewe taarifa za mvua za wastani, Juu ya wastani au chini ya wastani yataendelea kuwa hivyo japo uwezekano wa kuwepo jua upo kutokana na ongezeko la joto.
Dkt. Kijazi ameongeza kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kutoa taarifa za hali ya hewa zenye uhakika na kusema utabiri wa msimu wa vuli mwaka jana,TMA ilitabiri kwa usahihi uliofikia kiwango cha asilimia 85.8.
Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kutambua umuhimu wa TMA na kuboresha mashine za kufanyia utabiri na kuajiri wataalamu ambao kwa pamoja wanashirikiana kutumia mitambo ya kisasa kuufamisha umma.
Aidha, Dkt. Kijazi ameongeza kuwa wako katika mkakati wa kuongeza vitu vya hali ya hewa nchi nzima ambapo wataanza na Dar es Salaam ambako kuna vituo viwili tu huku mahitajia yakiwa ni vituo zaidi ya 10
WABUNGE WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Pichani
kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero
Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
Wabunge
watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa
mahakama ya Kisutu hivi punde kwa tuhuma za rushwa,Wabunge hao kama
waoenekanavyo pichani ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa
Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor
Mwambalaswa
REA WAJIBU MSAADA WA MCC
Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania
Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha
msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania
kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar
na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania
iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na
haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REA‘ Lutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA
haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za
serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya
fedha zote tunazofanyia kazi na hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’
>>>’Shughuli
za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi
kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekcuhablog
BAADA YA MCC NA HAWA WENGINE WAMETANGAZA
Baada ya MCC, hawa ni wengine waliotangaza kusitisha misaada kwa Tanzania kisa uchaguzi wa Znz
March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4
kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa
uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria
mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo >>> ‘kundi
la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha
ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa
shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada
kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa‘
‘Karibu theluthi moja ya bajeti
ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za
hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya‘ – BBC SWAHILI.Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
Wednesday, March 30, 2016
AMKA NA MAGAZETI NA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC TANGA
Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Asilia Cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi ni mabingwa wa kutibu magonjwa na hutoa ushauri wa uhakika. M,kombozi pia wako na vifaa vya kisasa vya kupimia mwili mzima. Wapo Tanga barabara ya 12 Ngamiani Tanga. simu 0654 361333
ABIRIA WA NDEGE APIGA PICHA MTU ANAEDAIWA KUWA MTEKAJI
Selfie ya Egyptair
Picha hiyo ya Ben Innes ,akitabasamu karibu na mtuhumiwa huyo katika ndege hiyo ya EgyptAir imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
Innes anayeishi Aberdeen pia aliliambia gazeti la Jumapili la Sun kwamba alitaka kuonyesha tabasamu mbele ya shida.
Alisema kuwa picha hiyo iliochukuliwa na mfanyikazi mmoja wa ndege hiyo ilikuwa ''selfie bora zaidi''.
Ndege hiyo ilikuwa ikibeba abiria 55,ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo.
Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.
UMMY MWALIMU AKEMEA WANAOJICHUKULIA SHERIA MIKONONO
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara
Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia
ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
………………………………………
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia
watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.
Amevitaka
vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo
hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa
kipato cha chini.
Mhe
Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Amewaonya
wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli
na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma
kwa kujichukulia sheria mkononi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo
kuzungumza na wafanyakazi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya hospitali
kufuatia tukio la mwananchi kumpiga daktari.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyefika hospitalini
hapo.
Mh.
Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na
mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula wakimsikiliza Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Mh. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja mbalimbali za madktari wa hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akikagua neti ya mmoja wa mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akifurahi kumuona mmoja wa watoto aliyezaliwa katika wodi ya wazazi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada ya kufanya
mazungumzo na watumishi wa hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akifurahi jambo na mmoja wa kina mama alipotembelea wodi ya wazazi
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungukia baadhi ya maeneo ya hospitali hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)