Tuesday, March 22, 2016

MRIPUKO YAIKUMBA BRUSSLS




 Moshi umeonekana ukitoka kwenye moja ya majumba katika uwanja huo

Milipuko miwili imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels.

Moshi umeonekana ukitanda angani kutoka kwa moja ya majengo katika uwanja huo.

Serikali ya Ubelgiji imethibitisha kwamba kunao watu waliojeruhiwa lakini haijasema idadi.

Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa kutoka uwanja huo kukatizwa.

Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipua

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kuna watu wamejeruhiwa katika ukumbi wa kuhudumia watu wa safari za kuondoka nchini na kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.

Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.

Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.

Uwanja wa ndege wa Zavantem kwenye picha iliyopigwa Desemba 2014
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.
Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.

No comments:

Post a Comment