Tuesday, March 15, 2016

MAJIMAREFU NYOTA YAKE YAZIDI KUNG'AA KOROGWE VIJIJINI, APOKEWA KAMA MFALME

 Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stivin Ngonyani Al maarufu Majimarefu, akipokewa kwa furaha na bibi wa Kwagunda alipofika kuhutubia wananchi wa kata hiyo kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wao.
Majimarefu aliahirisha kufanya mkutano kata hiyo baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa kuwa mgonjwa hivyo kusema kuwa haitokuwa vyema kufanya mkutano huo Ilhali kiongozi mwenyeji akiwa anauguwa.
Hata hivyo Mbunge huyo alitakiwa kuwakonga nyoyo wakazi wa Kwagunda kuwahutubia kwa dakika mbili tu ili kuweza kuisikia sauti yake na kutoa nasaha ya maneno mawili.
Baada ya kuombwa Majimarefu alipanda jukwaani na kuwaeleza kuwa anawashukuru kwa kumchagua tena kwa kura nyingi ambapo kata hiyo iliongoza kwa kumpa kura nyingi.
Alisema yuko pamoja nao bega kwa bega na atahakikisha miradi yote ambayo kwa jitihada zake ameisogeza anaisimamia yeye pamoja na viongozi wenzake hivyo kutaka kuungwa mkono.
Alisema Mradi wa Umeme wa Rea na usambazaji maji kila kaya atahakikisha inafanikiwa.



 `

No comments:

Post a Comment