Wednesday, March 9, 2016

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI SEIF SHARIIF HAMAD

 MAGUFULI AMJULIA HALI KATIBU MKUU WA CUF AMBAYE PIA NI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD JIJINI DAR ES SALAAM.

SEIF1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
SEIF2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
SEIF3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment