Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE wa
jimbo la Korogwe Vijijini (CCM), Stivin Ngonyani maarufu Majimarefu, amewataka
wananchi jimboni humo kujiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kupata
matibabu bure.
Akizungumza katika mikutano yake ya
kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa mara ya pili kuwa Mbunge wao kata ya
Lewa na Hale, Majimarefu alisema kila kaya ihakikishe imejiunga na mifuko ya
Hifadhi ya Jamii na kuweza kufaidika na huduma ya matibabu bure kwa gharama
kidogo.
Alisema gharama ya matibabu na
madawa madukani iko juu ambapo watu wengi hawana uwezo wa kumudu kutokana na
vipato vyao hivyo ni wajibu wa kila mtu kutambua kuwa kujiunga na mifuko ya
Jamii inaweza kuondoa ukali wa maisha
mmoja ndani ya familia wakati akiugua.
“Ndugu zangu wananchi wapiga kura
wangu tutambue kuwa kuna mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ukijiunga unapata
matibabu bure pamoja na wenza si zaidi
ya wanne” alisema Majimarefu na kuongeza
“Lakini niseme kufanikisha hili
nitazungumza na hiyo mifuko ya jamii kuja kwenu kuwapa elimu kwanza ili
mutambue umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii” alisema
Akizungumzia umuhimu wa kujiunga na
vikundi vya Ujasiriamali, Majmarefu aliwataka wanawake na vijana kuunda vikundi
ili kufaika na mikopo yenye riba nafuu na kuweza kutunisha mifuko yao.
Alisema vikundi viko na faida nyingi
ikiwemo kupata mikopo na misaada hivyo kuwataka makundi hayo kufanya hivyo
ambavyo pia itavutia watu wengine jambo ambalo litapunguza umasikini na watu
wasio na kazi.
“Watu wengi hawatambui kuwa vikundi vya
ujasiriamali ndivyo vinavyowatoa kimaisha, ukweli ni kuwa kujiunga kunafaida
nyingi ikiwemo mikopo katika taasissi za fedha na hata Serikali” alisema Mbunge
huyo
Aliwataka watu kufanya kazi na
kujuwa wajibu wake pamoja na kuzitumia rasilimali zilizoko ikiwemo kilimo cha
chai na mbogamboga na matunda na kusema kuwa masoko yapo.
Alisema wafanyabiashara wako huru
kutafuta masoko likiwemo la pamoja la
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hivyo kuwataka kulitumilia kwani
litawawezesha kutangaza biashara zao na kubadilishana uzoefu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment