Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara
Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia
ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
………………………………………
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia
watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.
Amevitaka
vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo
hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa
kipato cha chini.
Mhe
Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Amewaonya
wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli
na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma
kwa kujichukulia sheria mkononi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo
kuzungumza na wafanyakazi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya hospitali
kufuatia tukio la mwananchi kumpiga daktari.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyefika hospitalini
hapo.
Mh.
Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na
mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula wakimsikiliza Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Mh. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja mbalimbali za madktari wa hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akikagua neti ya mmoja wa mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akifurahi kumuona mmoja wa watoto aliyezaliwa katika wodi ya wazazi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada ya kufanya
mazungumzo na watumishi wa hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akifurahi jambo na mmoja wa kina mama alipotembelea wodi ya wazazi
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungukia baadhi ya maeneo ya hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment