Thursday, March 10, 2016

WAKWEPAJI ULIPAJI KODI KUKOMESHWA

Kama na wewe unakwepa kulipa kodi hili likufikie sasa kutoka Wizara ya Fedha


Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kwaajili ya kusupport mamlaka ya mapato katika kuongeza kipato nchini na kuongeza nguvu katika kuzuia mianya ya ukwepaji kodi kwa Watanzania.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema>> ‘Serikali ya Kifalme ya Norway imetoa msaada kwa Tanzania katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kwamba tunaweza kuzuia wanaokwepa kulipa kodi
Wizara ya fedha tunataka kuondoka kutoka katika bajeti ya utegemezi na kwenda katika bajeti ya kujitegemea, lakini hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato
Kwahiyo tunaishukuru sana Serikali ya Norway kwa msaada huu na pia tunawaahidi tutazitumia vizuri katika kuimarisha mamlaka yetu ya mapato na kazi zake kwa ujumla
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment