Thursday, March 10, 2016

MAN UNITED YALALA KWA LIVEPOOL

Manchester United wamepokea kichapo Anfield dhidi ya Liverpool


Usiku wa March 10 michuano ya Europa League iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa Barani Ulaya, Uingereza kulikuwa kuna mchezo wa kuvutia zaidi baina ya Liverpool dhidi ya Manchester United katika dimba la Anfield.
12822366_477920652413610_1339610887_n
Roberto Firmino akishangilia goli
Takwimu za vilabu hivi kabla ya mchezo huu kupigwa , Man United alikuwa na takwimu nzuri licha ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kwa mujibu wa mechiza mwisho za Manchester United na Livepool walivyokutana, Man United alikuwa kashinda mara nne na Liverpool mara moja
Hata hivyo takwimu hizo hazikuwa na msaada wowote kwa Man United  kwani vijana wa Jurgen Klopp  walifanikiwa kuifunga Man United kuanzia dakika ya 20 kupitia kwa Danny Sturridge kwa mkwaju wa penati, kabla ya dakika ya 73′ Roberto Firmino kupachika goli la pili lililoimaliza Man United na kufanya mchezo umalizike kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

No comments:

Post a Comment